November 21, 2016Kikosi cha Boko Vetarani kimeionyesha njia za soka Bunju Veterani kwa kuibanjua kwa mabao 6-0 katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam, jana jioni.

Ushindi huo wa Boko Veterani maarufu kama BBV, umeifanya kuweka rekodi ya kucheza mechi tano bila ya kupoteza hata moja.

Kabla ya mechi dhidi ya Bunju, ilikuwa imeshinda dhidi ya Tabora Veterani, BOT Veterani, Mbezi Veterani na  Lugalo Veterani.


Kiungo  Lazaro  Ngimba ndiye alianza kwa kuihadaa ngome ya Bunju na kutoa pasi mujarab kwa Bruce Mwile aliyetikiza nyavu na Boko Veterani kuongoza kwa bao moja.

Huku ikionekana kama Bunju wamechanganyikiwa, BBV waliongeza mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kuwaweka Boko kwenye kona ya kuwamaliza kabisa.

Mabao mengine ya BBV ambao walikuwa wakiachia pasi za kugusa, yalifungwa na Lazaro, Holombe Jr, Hebron Malakasuka huku Bruce Mwile akiwa ametupia hat trick kama ile ya Cristiano Ronaldo wakati Madrid ikiivaa Atletico Madrid pale Vicente Calderon.

Kikosi cha BBV walioanza na wengine kutokea benchi:
 Shabani Dihile,
Mango, Msaki, Robert, Kairuki,
Lazaro, Rodrick Mwambene, Deo Ringia, Horombe, Mawinga Ole aka Aguero, Richard, Chief Ndabile 
Bruce, Edwin aka Mavugo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV