November 6, 2016


Bila ya kuwa na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu ambaye alikuwa tegemeo, TP Mazembe ya DR Congo imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jana kuifunga MO Bejaia ya Algeria kwa mabao 4-1 katika mchezo wa marudiano wa fainali.

Ulimwengu amemaliza mkataba wake na TP Mazembe na ana mpango wa kwenda kucheza soka barani Ulaya.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo jijini Lubumbashi, mabao ya washindi yalifungwa na Jean Kasusula dakika ya saba, Rainford Kalaba dakika ya 44 na 62 na Jonathan Bolingi dakika ya 77. Bao la MO Bejaia lilifungwa na Sofiane Khadir dakika ya 75.

Ushindi huo, umeiwezesha Mazembe kupata ushindi wa jumla wa mabao 5-2 baada ya awali timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 nchini Algeria.

Huu ni ubingwa wa kwanza wa Mazembe katika Kombe la Shirikisho licha ya kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika mara tano katika miaka ya 1967, 1968, 2009, 2010 na 2015.

Mazembe na MO Bejaia zilikuwa kundi moja la A sambamba na Yanga na Medeama ya Ghana ambazo zilitolewa katika hatua hiyo ya robo fainali.

Hata hivyo, Mazembe iliyo chini ya Kocha Hubert Velud, ilicheza bila ya Mtanzani Thomas Ulimwengu ambaye yupo nchini akiwa amemaliza mkataba na timu hiyo.

VIKOSI
TP Mazembe:
 Sylvain Gbohouo; Kasusula, Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Roger Assale, Merveille Bope, Jonathan Bolingi, Kalaba (Kanda 84), Daniel Adjei (Koffi 76), Solomo Asante (Traore 69), Christian Luyindama.


MO Bejaia: 
Chamseddine Rahmani; Ismail Benettayeb (Belkacemi 67), Malek Ferhat (Yesli 61), Faouzi Rahal, Faouzi Yaya, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Mohamed Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali na Yassine Salhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV