November 6, 2016


Bondia Francis Cheka ameibuka na kumuomba Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kuwakomboa kutoka mikononi mwa mapromota wababaishaji.

Cheka ametupia ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, akimuomba Nape awakomboe kwa kuwa kumekuwa na mapromota ambao hushikilia pasi zao za kusafiria huku wakijua si sahihi.


"Waziri wangu, embu angalia mapromota wanavyo tutesa, wanakaa na Viza na Passport zetu, ambayo ni haki zetu kama raia," aliandika Cheka.

"Tunakosa mapambo ya nje, Waziri wa Michezo tukomboe ili tukuletee mikanda mingi, pesa za kigeni, heshima na tuitangaze zaidi nchi yetu huko nje."

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV