November 27, 2016


CRUZ

Bondia Orlando Cruz amekutana na kipigo kikali kutoka kwa Terry Flanagan ambaye alimuangusha na kushinda kwa TKO.

Cruz amekutana na kipigo hicho ikiwa ni mara ya kwanza tokea atangaze yeye ni shoga mwaka 2012 lakini bondia mwenzake amemshambulia hadharani.


Peter Fury ambaye ni mmoja wa mabondia nyota na Frankie Gavin pia, wameandika kwenye mitandao ya kijamii wakieleza kipigo cha Cruz kinaonyesha tofauti ya mwanamke kamili, dhidi ya asiyekamilika.


Maneno ya mabondia hao wawili kupitia mtandao wa Twitter yanaonyesha kiasi gain walivyokerwa na uamuzi wa Cruz kujitangaza hadharani kwamba yeye ni shoga.


Wakati alipofanya hivyo, mabondia wengi walipinga wakionyesha wameingiliwa kwa kuwa inaonekana mchezo wa wanaume kamili, sasa wako ambao wameanza kufanya tabia hiyo mbaya na ya hovyo kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV