November 28, 2016Beki wa kati wa Yanga, Vincent Bossou amekwenda nchini Vietnam ikielezwa anamsindikiza mdogo wake anayekwenda kusaini mkataba wa kucheza soka nchini humo.

Lakini taarifa nyingine, zimeeleza Bossou amekwenda kufanya majaribio kimyakimya bila ya kuwaeleza Yanga.


Bossou amekiri hatakuwa katika kikosi cha Yanga kinachoanza mazoezi yake ya kwanza chini ya Kocha George Lwandamina jijini Dar es Salaam.
“Mimi nitarudi nchini Desemba 3, siku sita baada ya kambi kwa ajili ya kujiunga na wenzangu pamoja na kocha mpya George Lwandamina, nitakosekana kwa siku hizo kwa sababu nitasafiri kuelekea nchini Vietnam.
“Naenda kumsindikiza ndugu yangu kusaini mkataba na moja ya timu za huko pamoja na mimi mwenyewe kumalizana na timu ambayo nitaenda kujiunga nayo baada ya mkataba wangu kumalizika hapa Yanga,” alisema Bossou.

Lakini taarifa nyingine zimesema, Bossou alizuiwa kuingia Vietnam kwa kuwa hakuwa na barua ya Yanga inayomruhusu kwenda Vietnam kufanya majaribio.

Jambo lililomlazimu kuwasiliana na viongozi wa Yanga na kuwaeleza nia yake ya kwenda Vietnam, ikiwa maelezo yanapishana na yale aliyoyatoa awali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV