November 28, 2016Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, jana Jumapili alishindwa kurejea nchini kujiunga na timu yake kwa kile kilichoelezwa kwamba anamuuguza mama yake nyumbani kwao, Yaoundé, Cameroon.

Leo Jumatatu, Simba inatarajiwa kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Desemba 17, lakini Omog atakosa wiki ya kwanza ya maandalizi hayo.

Huku Omog akikosekana, kikosi hicho kitakuwa kikinolewa na kocha msaidizi, Jackson Mayanja, raia wa Uganda ambaye alitarajiwa kutua nchini jana Jumapili akitokea kwao Uganda.

Mratibu wa Simba, Abass Ally, amesema kuwa, Omog anatarajiwa kutua nchini Desemba 2, ikiwa ni siku tano tangu kikosi hicho kianze mazoezi.

“Omog atarejea nchini Desemba 2 kuungana na timu kwani kwa sasa yupo kwao Cameroon akimuuguza mama yake, hivyo Mayanja atakuwa akisimamia mazoezi kwa siku ambazo yeye hayupo.


“Mambo mengine yote yataenda kama yalivyopangwa, tunaanza maandalizi ya mzunguko wa pili, hivyo wachezaji wote watatakiwa kuwepo,” alisema Ally.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV