Kuelekea
kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018, Brazil imeifunga Argentina mabao 3-0
katika mchezo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo Ijumaa.
Brazil
ambayo ilipoteza makali katika miaka ya hivi karibuni, imepata ushindi huo
kupitia kwa mabao ya Philippe Coutinho, Neymar na Paulinho.
Argentina
ikiongozwa na nahodha wake, Lionel Messi ilishindwa kufurukuta licha ya kuchezeha
kikosi kamili, hivyo imejiweka katika mazungira magumu ya kusonga mbele katika
ukanda wa Amerika Kusini.
Kwa sasa
Argentina inashika nafasi ya sita kati ya 10 zinazowania nafasi ya kusonga
mbele katika kusaka tiketi ya kucheza michuano hiyo mikubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment