November 11, 2016

Wakati mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ukifikia ukingoni jana, uongozi wa Azam FC umeamua kumpeleka katika kikosi cha vijana cha timu hiyo Muivory Coast, Pascal Wawa ili kulinda kiwango chake kama ilivyokuwa kwa kiungo wa Manchester United, Mjerumani, Bastian Schweinsteiger.
Wawa


Licha ya kupelekwa kwenye kikosi cha timu ya vijana, beki huyo tayari ameshaweka bayana kuwa hana mpango wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kufuatia madai ya kukataliwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Zeben Hernandez huku mkataba wake ukimalizika mwezi huu.

Schweinsteiger



Hali iliyomkuta Wawa, ni kama ilivyokuwa kwa Schweinsteiger ambaye kocha wake, Jose Mourinho aliamua kumpeleka katika kikosi cha vijana kutokana na kutokuwa kwenye mipango yake.

Taarifa za uhakika ambazo Championi Ijumaa linazo ni kuwa beki huyo alipelekwa kuanza kufanya mazoezi na timu ya vijana kufuatia kutokuwa na maelewano mazuri na kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumueleza wazi kwamba hamuhitaji katika kikosi chake.

“Wawa hawezi kubaki Azam kabisa kwa sababu ametakiwa kufanya mazoezi na kikosi cha timu ya vijana ili kulinda kiwango chake kwa muda uliobaki kabla ya kuondoka kwa mujibu wa mkataba wake jinsi ulivyo.

“Anafanya mazoezi na timu ya vijana karibu siku zote timu inapokuwa na ratiba ya kufanya hivyo akitokea kwake Kijichi anapoishi.”

Alipotafutwa Wawa alisema: “Ni kweli nafanya mazoezi na timu ya vijana kwa sasa.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic