November 26, 2016Ikiwa na wewe uliidharau Ndanda FC ujue imekula kwako kwani timu hiyo ya mkoani Mtwara ipo katika mipango mikali ya kuwasajili wachezaji nyota watano ili kukiongezea nguvu kikosi chao katika Ligi Kuu Bara.

Ndanda inayotumia Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo Mtwara Mjini kwa ajili ya mechi zake za ligi hiyo, ipo nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 19.

Klabu hiyo maarufu kama Ndanda Kuchele yaani Ndanda Kumekucha, inataka kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakaoanza Desemba 17, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Ndanda, Idrissa Bandari ameliambia Championi Jumamosi kuwa: "Kiukweli kwa sasa tupo katika mazungumzo na wachezaji watano kwa ajili ya kuwasajili ili watuongezee nguvu.

“Tunataka tufanye vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, siwezi kuwataja kwa majina wala timu wanazotoka kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea, tutakapokamilisha kila kitu tutawataja.


“Unajua mambo ya usajili yanavyokwenda maana bado tunazungumza sasa naweza kuwataja na kuharibu kila kitu ili tuna uhakika wa kuwasajili wote,” alisema Bandari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV