November 25, 2016Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss Afrika mwaka 2016,  Julitha Kabete, kesho Jumamosi  atapanda jukwaani moja na washiriki wenzake 18 kuwania taji la mrembo wa michuano hiyo linalofanyika nchini Nigeria.

Mashindano haya yatakayofanyika nchini Nigeria, jimbo la Cross River, mjini Calabar mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajipatia kitita cha dola za Kimarekani 25,000 ni sawa na sh.milioni 52 ya Tanzania na pamoja na gari jipya.


Mshindi  wa pili katika shindano hilo atapata kitita cha dola ya Kmarekani 15,000  ni sawa na sh.milioni 33 za Kitanzania na wa tatu  dola 10,000 ni sawa na sh.milioni 22.

Akizungumza na Gazeti hili, mshiriki huyo alisema kikubwa ni Watanzania wenzake kumuombea dua haweze kushinda taji hilo.

Kabete alisema kuna upinzani mkali, lakini nae kwa upande wake anajiamini anauwezo mkubwa wa kufanya vizuri na kubeba taji la shindano hilo.

"Nina nafasi ya kufanya vizuri, kikubwa naomba dua zetu Watanzania wenzangu, niweze kufaya vizuri na kubeba taji"alisema Kabete.

Mrembo huo ameenda kushiriki shindano hilo alikiwa chini ya kampuni ya Millen Magese  Group (MMG),  chini ya mkurugenzi wake Happiness 'Millen' Magese, anayefanya shughuli zake za mitindo nchini Marekani.


 .


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV