November 26, 2016

LUNYAMILA

Soka ni raha, maana zaidi ya timu nane za maveterani kutoka jijini Dar es Salaam pamoja na mkoani Pwani, kesho Jumapili zitaonyesha ubabe katika bonanza litakalofanyika Bagamoyo kwenye Uwanja wa Mwanakalenge.

Bonanza hilo limeandaliwa na Temboni Veterani ya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwakutanisha nyota wa zamani waliopata kutamba na timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara zikiwemo Simba na Yanga.

Vincent Peter ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni msemaji wa Temboni Veterani, alizitaja timu zitakazopambana katika bonanza hilo kuwa ni Kibamba, Golani, Corner na Kibangu ambazo zote ni kutoka Dar es Salaam.

“Mbali na timu hizo pia kutakuwa na timu nyingine kutoka Bagamoyo, katika bonanza hilo hakuna kiingilio, tunawaomba watu wajitokeze kwa wingi waje kuwaona nyota mbambali waliotamba na timu za Simba na Yanga na nyingine za ligi kuu.


“Wachezaji kama Edibily Lunyamila, Nico Nyagawa, Jemin Kiiza, Ramadhan Wasso, Steven Nyenge na Henry Freeman watakuwepo uwanjani wakionyesha ufundi wao, pia kutakuwa na burudani ya muziki,” alisema Peter.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV