November 22, 2016


Kiungo mkabaji wa CSKA Moscow ya Russia, Roman Eremenko amefungiwa miaka miwili baada ya kubainika anatumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Eremenko amepatikana na hatia hiyo baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen iliyopigwa Septemba 14, mwaka huu na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), limepitisha na kuitangaza adhabu hiyo.


Kutokana na adhabu hiyo, Eremenko raia wa Finland ataukosa msimu wote ujao pia utakaofuata nusu msimu.


Bodi ya Uefa ya Uthibiti, Hadhi na Nidhamu imesema itaendelea kufanya uchunguzi kama kawaida kwa wachezaji mbalimbali kama ambavyo imekuwa ikifanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic