November 22, 2016Uongozi wa klabu ya Yanga, umeanza mazungumzo ya kuhakikisha wachezaji wake waliomaliza mkataba na wanahitajika, inaingia nao mikataba mipya.

Baadhi ya wachezaji waliomaliza mikataba yao ni pamoja na Donald Ngoma na Vincent Bossou ambao wako mapumzikoni.

Habari za kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, tayari mazungumzo kati ya uongozi na wachezaji hao yalianza kitambo.

“Mambo mengi Yanga wanafanya kimyakimya, hivyo mtu anaweza kusema asijue kinachoendelea.

“Kama kuna mchezaji ataamua kuondoka, basi labda kuna kitu kingine lakini Yanga wanajua wanachokifanya na kila kitu kinakwenda kwa mpangilio,” kilieleza chanzo.
Wachezaji wengine ambao mikataba yao inakwenda ukingoni ni pamoja na Deus Kaseke pia Matheo Anthony pamoja na Malimi Busungu ambao hawakutumika sana katika mzunguko wa kwanza.


Angalau Anthony alipata nafasi ya kuingia lakini Busungu, mambo hayakuwa mazuri ikafikia akaamua kukaa kando.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV