November 21, 2016Baada ya Mfaransa, Patrick Liewig kuachana na Stand United, sasa imeelezwa mikoba yake itachukuliwa na Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco ambaye tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo.

Morocco ambaye amewahi kuzinoa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Zanzibar, ataungana na Athuman Bilal ‘Bilo’ katika kuiongoza timu hiyo inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa katibu wa klabu hiyo, Kennedy Nyangi, ni kwamba, baada ya kuwa na mazungumzo na makocha wengi, lakini wamefikia maamuzi ya kukaa chini na kumalizana na kocha huyo.

“Tulikuwa na mazungumzo na makocha wengi ili kuziba nafasi ya Liewig, kati ya hao tumeona Hemed Morocco anafaa kuwa kocha wetu mkuu, kilichobaki kwa sasa ni kuona ni kwa namna gani tunamalizana naye,” alisema Nyangi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV