November 28, 2016Huku timu za Yanga na Simba zikianza kambi zake leo Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, wapinzani wao Azam FC bado wapo majumbani wakisubiri kurejea kwa kocha wao Mhispania, Zeben Hernandez, Desemba 5, mwaka huu.

Zeben kwa sasa yupo kwao Hispania alipokwenda mapumziko kabla ya kurejea nchini kuendelea na kibarua chake cha kuiongoza timu hiyo kwenye mzunguko wa pili ambao umepangwa kuanza Desemba 17.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema licha ya wenzao hao kuanza kambi mapema, kwa upande wao wanamsubiria kocha wao Zeben arejee kutoka kwao Hispania, ndipo waanze kambi yao.

“Kocha wetu atatua nchini Desemba 2 na kambi rasmi tunatarajia kuanza siku tatu mbele yaani Desemba 5, ambapo tunaamini tukirejea tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri, kwa sababu kikosi kimeimarika tofauti na mara ya kwanza ilivyokuwa.


“Akishatua hapa nchini ndipo mambo mengine yataendelea ukiwemo usajili wa wachezaji ambao tunawataka kabla ya kufungwa dirisha hili, ambao tuliusimamisha kwa sababu yeye hakuwepo nchini,” alisema Jaffar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV