November 16, 2016

MBAO FC


Baada ya dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara kufunguliwa jana Jumanne, uongozi wa Mbao FC ya jijini Mwanza umeweka wazi mikakati yake ya kukiboresha kikosi chake kwa kutaka saini za wachezaji kama Haruna Niyonzima wa Yanga na Laudit Mavugo wa Simba.

Mbao FC ambayo msimu huu inashiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza, ilianza kwa kusuasua katika ligi hiyo lakini baadaye ilikaa sawa na kuanza kufanya vema na kufanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza hivi karibuni ikiwa nafasi ya 12 na pointi 16.


Katibu wa klabu hiyo, Richard Athanas, amesema, tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Etiene Ndairagije, raia wa Burundi, amependekeza kuletewa nyota watatu lakini akasisitiza kuwa wawe na uwezo kama Niyonzima na Mavugo ambao anaamini ndiyo wachezaji walifanya vizuri katika mzunguko huo.

“Kocha amekuwa akipendekeza sana wachezaji wenye uwezo kama wa nyota hao, endapo atawapata atakuwa ameboresha safu yake ya kiungo na usambuliaji kwa kiasi kikubwa, hivyo uwezekano wa kumaliza ligi akiwa katika nafasi nzuri za juu atakuwanao mkubwa.


“Mbali na nafasi hizo, pia amependekeza mlinzi wa kati mwenye uwezo wa kuzuia hatari wakati wowote ule, kutokana na hali hiyo tunajipanga ili tuweze kuanza kuyafanyia kazi mapendekezo yake hayo,” alisema Athanas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV