November 5, 2016


Ligi ya Vijana ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) wenye umri wa chini ya miaka 20, inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 mwaka huu kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwa timu za vijana za Kagera Sugar na Young Africans ya Dar es Salaam kuchuana siku hiyo.

Timu hizo ambazo zimepangwa kundi A, zitaanza mchezo wao siku hiyo saa 10.30 jioni (16h30) ikiwa ni baada ya shamrashamra za uzinduzi wake. Kwa kuwa itakuwa ni uzinduzi, basi siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja tu, lakini kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi ya TFF kwa siku kutakuwa na michezo miwili kwa tofauti ya saa – mchana na jioni.

Mbali ya Kagera Sugar na Young Africans, timu nyingine ambazo zitakuwa kwenye kundi hilo la A ni Stand United na Mwadui za Shinyanga ambazo zitacheza siku inayofuata (Novemba 16, 2017) saa 10.30 jioni na kwa kukamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo, Novemba 17, mwaka huu Azam itacheza na Mbao FC katika mchezo utakaopigwa saa 8.00 mchana (14h00) kabla kuzipisha Toto Africans na African Lyon saa 10.30 jioni.

Kwa upande wa Kundi B ambalo kituo chake rasmi kitakuwa Dar es Salaam, Simba itafungua dimba na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini - mchezo utakaonza saa 8.00 kabla ya kuzipisha timu za JKT Ruvu na Ruvu Shooting kucheza saa 10.30 jioni siku hiyo hiyo.

Ili kukamilisha mzunguko wa kwanza, siku inayofuata Novemba 17, mwaka huu Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City saa 8.00 mchana (14h00) wakati Majimaji itacheza na Mtibwa saa 10.30 jioni.

Ligi hiyo ya mkondo mmoja, hatua ya makundi inatarajiwa kufikia ukomo Desemba 12, 2016 ambako timu nne vinara kutoka katika kila kundi zitapangiwa ratiba mpya na kituo ili kutafuta bingwa wa msimu kwa timu za vijana. Kituo hicho kitatangazwa baada ya kumalizika hatua ya makundi hapo Desemba 12, mwaka huu.


Ujio wa ligi hiyo ni utekelezaji au kukidhi matakwa ya maelekeo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kategori ya uwepo wa timu za vijana zinazoshindana mbali ya kupata huduma za shule na matibabu kwa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic