November 16, 2016


Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema anaijua vizuri Simba na mara ya mwisho anaikumbuka alipoipa kichapo cha mabao 3-0.

Zesco aliyokuwa anainoa iliichapa Simba kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki miaka miwili iliyopita.

Baada ya kipigo hicho, Kocha Zdravko Logarusic akatimuliwa kazi na uongozi wa Simba.

Lwandamina ambaye alikuwa mafichoni ambako uongozi wa Yanga ulimuweka kabla ya kuibuliwa na gazeti la CHAMPIONI, amesema amekuwa akiisikia Simba lakini kuijua zaidi ni hiyo mechi waliyocheza.

SALEHJEMBE: Unawajua Simba?
Lwandamina: Ndiyo, kwa maana ya kuwasikia lakini nimewahi kuwaona na kucheza nao.

SALEHJEMBE: Unawazungumziaje?
Lwandamina: Najua ni timu kubwa, wapinzani wa Yanga. Najua ina mashabiki wengi pia, maana tulipocheza nao na kuwafunga mabao 3-0, niliona mashabiki wao walivyojisikia vibaya.

SALEHJEMBE:Nakumbuka ilikuwa ni mechi ya kirafiki kwenye Simba Day?

Lwandamina: Ndiyo, nakumbuka baada ya kuwafunga, walimfukuza yule kocha wao Mzungu (Zdravko Logarusic).

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV