November 29, 2016Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina amesema ameanza kazi yake vizuri akiwa anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Hans van der Pluijm.

Lwandamina amesema, siku ya kwanza tu imemuonyesha mwanga kwamba mambo yatakwenda vizuri lakini ni lazima wafanye kazi kwa juhudi.

“Tutafanya kazi kwa juhudi na ushirikiano wa juu kabisa. Tumeanza vizuri na umeona morali ya wachezaji iko juu,” alisema.


Yanga ilianza mazoezi yake kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam na Pluijm na Lwandamina wote walionekana wakiwa kazini pamoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV