November 29, 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema ushirikiano wa karibu kati ya vyombo vya habari vya Tanzania na vile vya China, vinaweza kuongeza ufanisi katika fani ya habari.

Waziri Nape aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa hafla ya uzinduzi wa kongamano la waandishi wa habari ambalo lilihudhuriwa na waandishi kutoka Tanzania na China wapatao 30.


"Wachina sisi ni ndugu zetu, kama ushirikiano kati yao na sisi utadumishwa. Utasaidia ukuaji wa haraka wa tasnia ya habari.

"Tunaweza kualikana kwa ajili ya mafunzo na mambo mbalimbali kwa nia njema," alisema.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Chama cha Ukomunisti, Sun Zhijun pia alihudhuria na kuhamasisha suala hilo la ushirikiano na mafunzo.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic