November 25, 2016Kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina ametua Yanga na kukabidhiwa jukumu la kuitoa Yanga ilipofikia.

Lwandamina raia wa Zambia ametambulishwa leo rasmi na Makamu wa Rais wa Yanga, Clement Sanga mbele ya waandishi wa habari.

“Tunaamini kocha atatusaidia kutoka hapa tulipofikia na kusonga mbele hasa katika michuano ya kimataifa,” alisema.

Lwandamina atakuwa akifanya kazi na Hans van der Pluijm ambaye sasa ni mkurugenzi wa ufundi.

Pluijm ambaye amepanda cheo, aliifikisha Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.


Awali Yanga hawakutaka kumzungumzia kocha huyo hadi blog ya SALEHJEMBE ilipomuibua mafichoni katika hoteli moja ya kitalii jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV