November 7, 2016


Hatimaye Kocha George Lwandamina amemalizana na klabu ya Zesco ambayo ameipa mafanikio makubwa.

Lwandamina ameachia ngazi rasmi kuinoa Zesco ambayo mkataba wake ulikuwa unaisha Januari 2017.

Akizungumza kutoka Zambia, Lwandamina amethibitisha kuachia ngazi katika klabu hiyo.

"Ni kweli, tumemalizana vizuri kabisa na mambo yamekwenda kitaalamu," alisema.

Kuhusiana na kutua Yanga, Lwandamina amekubali kuwa anakuja nchini lakini hakutana kuweka wazi.

"Baada ya hapa Zesco, sasa naelekea katika nchi nyingine ya Afrika. Nipe siku moja nikupe jibu," alisema.

Lakini taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kocha huyo atafika nchini kesho usiku kwa ajili ya kumalizana na Yanga.

"Tunajua anakuja huko Tanzania kesho usiku, ndege yake inaonyesha hivyo," alisema wakala wake.


1 COMMENTS:

  1. Karibu Young African ufanye kazi na mabingwa wa kihistiria Tanzania.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV