Shughuli za mazishi ya bondia Thomas Mashali zitaanza kesho saa tano asubuhi kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Kamati ya mazishi iliyokutana leo na kuongozwa na Japhet Kaseba, Rashid Matumla, Emmanuel Mlundwa, Juma Mbizo na wengine, imefikia uamuzi huo kuwa Mashali ataagwa Leaders na mazishi ni makaburi ya Kinondoni.
Mashali ameuwawa na watu wasiojulikana na bado polisi haijaeleza nini hasa imepata.
Lakini taarifa zinasema alishambuliwa hadi kupasuliwa kichwa katika eneo la Tabata karibu kabisa na Kimara Bonyokwa.
Alikimbizwa katika Hospitai ya Palestina, lakini ikashindikana. Akahamishiwa Muhimbili ambako alipoteza maisha usiku wa kuamkia juzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment