Baadhi ya wanachama wa Yanga, wamepata ajali mbali ya gari.
Bahati nzuri, wote wamefanikiwa kutoka salama katika ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mwidu, wakiwa njiani kwenda Mbeya kuiwahi mechi kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City, kesho.
Baadhi ya viongozi waliokuwa katika gari hilo dogo aina ya Suzuki Vitara ni kamati ya mashindano na ya Utendaji ya Yanga, Omary Said, Bakili Makele na Seif Chuma walikuwa ndani ya gari hilo.
Makele amethibitisha wao kupata ajali hiyo na kusema wameamua kuahirisha safari.
“Tunashukuru Mungu sana, tumetoka salama ingawa ajali ilikuwa mbaya sana. Sasa tunarejea Chalinze ambako tutafanya taratibu nyingine,” alisema.
Salehjembe, inatoa pole kwa wanamichezo hao kwa ajali mbaya iliyowakuta. Mungu awape nguvu zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment