November 16, 2016


Lionel Messi ameowangoza wachezaji wa timu ya Argentina kususia kujibu maswali ya waandishi wa habari.

Messi amefanya hivyo baada ya kiungo wa timu hiyo, Lavezzi kutangazwa kwamba anatumia dawa za kulevya huku akijua ameitwa kwa ajili ya majukumu ya timu ya taifa.

Argentina iliitwanga Colombia kwa mabao 3-0 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia na kuamsha matumaini.

Messi alisema wachezaji wote wanaungana na hawatajibu swali lolote la waandishi wa habari huku akisisitiza wanataka kupewa heshima yao.


LAVEZZI ALIYEZUNGUSHIWA DUARA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV