November 2, 2016


Baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara, kiungo mchezeshaji wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amewatolea uvivu waliokuwa wakibeza kiwango chake kushuka akiwaambia waendelee kuchonga.

Kiungo huyo, alirejea uwanjani rasmi kwenye mechi dhidi ya Toto Africans na kuiwezesha Yanga kupata ushindi mnono kwenye michezo yote minne huku yeye akiwa uwanjani akicheza kwa dakika 90.

Mechi ya kwanza ni dhidi ya Toto ambayo walishinda mabao 2-0, Kagera Sugar 6-2, JKT Ruvu 4-0 kabla ya kuvaana na Mbao FC ambayo nayo waliifunga mabao 3-0.

Niyonzima amesema mengi yalizungumzwa wakati yupo nje akiwa na matatizo ya kifamilia yakiwemo kiwango chake kushuka, ndiyo sababu ya yeye kutoonekana uwanjani.
Niyonzima amewataka mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakibeza kiwango chake waendelee kuongea na wasikae kimya.

“Mbona siyasikii tena maneno yao waliyokuwa wanaongea mashabiki wa Yanga kuwa mimi kiwango changu kimeshuka baada ya kucheza mechi hizi nne za ligi tangu niliporejea rasmi uwanjani?

“Nikwambie kitu, nimepanga kuwanyamazisha kwa kuonyesha kiwango kikubwa kwenye kila mechi nitakayocheza ili kuhakikisha ninaipa matokeo mazuri timu yangu ya Yanga.

“Na nisingependa kupokea pongezi au sifa za mashabiki waliokuwa wakibeza kiwango changu, kwa sababu tangu mechi na Kagera napokea ujumbe mwingi wa pongezi kuwa nimecheza vizuri kati ya hao wapo waliokuwa wakibeza kiwango changu hapo mwanzo,” alisema Niyonzima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic