November 2, 2016


PONDAMALI

Dah! Kumbe Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ambaye amekataliwa kujiuzulu nafasi yake, alijua tangu kitambo kwamba atatimuliwa kazi kwani uongozi uliwataarifu mapema.

Anayethibitisha hilo ni kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali ambaye alisema mabadiliko katika benchi la ufundi la timu hiyo kila mtu alikuwa akijua hata Pluijm kwa sababu uongozi ulikuwa umewaambia.

Pondamali alisema kutokana na hali hiyo kwa upande wake yeye alikuwa ameshajipanga kukukabiliana na jambo lolote lile ambalo lingetokea kwani walishaambiwa.

PLUIJM

Alisema hata aliposikia kuwa kuna kocha mpya amekuja kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo kwa upande wake hakushangaa.

“Viongozi wote wa benchi la ufundi tulikuwa tunalijua hilo kuwa wote tutaondolewa kazini baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu na hata baada ya kutoka kwa hili la juzi sikushangaa.

“Hata hivyo, kwa upande wangu nilishajipanga siku nyingi baada ya kumalizika tu kwa mkataba wangu kwani kila nilipokuwa nikimwambia katibu nilikuwa sipati jibu la uhakika hapo ndipo nikaanza kujiandaa.


“Endapo itatokea sasa nimetimuliwa sitakwenda tena kufundisha soka ila nitatumia muda huo kujiimarisha zaidi katika fani yangu ya muziki ikiwa ni pamoja na kuzifanyia promo ngoma zangu,” alisema Pondamali

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic