Kocha Hans van der Pluijm amesema ataikumbuka klabu ya Yanga kwa mambo mengi sana kwa kuwa ataondoka akiwa bado anaipenda.
Pluijm raia wa Uholanzi mwenye makazi yake nchini Ghana, amesema Yanga ni moja ya klabu bora kabisa alizozifundisha.
“Nitaendelea kuikumbuka Yanga kwa kuwa kwangu ni familia, nakwenda kama binadamu yoyote.
“Natoa shukurani kwa Wanayanga wote na mechi ya mwisho ya mzunguko huu wa kwanza itakuwa ya mwisho kwangu,” alisema.
Pluijm anaondika Yanga na nafasi yake inachukuliwa rasmi na kocha Geirge Lwandamina raia wa Zambia.
0 COMMENTS:
Post a Comment