November 10, 2016

Aliyekuwa Msaidizi wa Rais wa TFF, Juma Matandika na aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano wa shirikikisho hilo, Martin Chacha, jana wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkiazi Kisutu jijini Dar na kusomewa shitaka la kuomba rushwa. 

Imedaiwa mahamakani hapo na mwendesha mashitaka wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa Takukuru, Leonard Swai kuwa mnamo Februari 4 mwaka huu washitakiwa waliomba rushwa ili waweze kupanga matokeo katika mechi iliyozikutanisha timu za daraja la kwanza Polisi Tabora na Geita Gold ili Geita ipande daraja na kufika Ligi Kuu.


Washitakiwa wote wawili walikana mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi. 

Wakili Swai alisema ushahidi umekamilika hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa novemba 30 mwaka huu mahakamani hapo. Washitakiwa hao wakati wakipandishwa kizimbani Matandika alisikika akiwachimbia mkwara mapaparazi waliokuwa wakimfotoa na kuwataka wamuache.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV