November 21, 2016Kesho Jumanne, Real Madrid itakuwa genii dimbani ikiivaa Sporting Lisbon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Cristiano Ronaldo atakuwa na raha zaidi kwa kuwa atakuwa anarejea nyumbani tena, lakini safari hii akiwa na kiatu maalum.
Viatu hivyo vimetengenezwa na Nike vikiwa na tarehe maalum inayoonyesha Agosti 6, 2003.

Agosti 6, 2003 ndiyo siku maisha ya Ronaldo yalipobadilika katika uwanja atakaocheza Jumanne wakati Manchester United walipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sporting Lisbon.

Baada ya mechi hiyo, Man United wakiwa wamelala kwa mabao 3-1, Kocha Alex Ferguson alimueleza Ronaldo kwamba anamhitaji ajiunge na Man United.


Mwaka 2009 aliondoka United na kujiunga Real Madrid ambayo kesho anakwenda nayo mjini humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV