November 21, 2016Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11.

Mkutano huo umeitishwa baada ya kikao cha kamati  ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa juzi. Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kamati ya utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya katiba ya Simba.


“Mkutano huo utakuwa ni mwendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyikaJulai 31, 2016,” alisema Manara.

Ingawa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari haijafungua kila kitu, lakini inaonekana mwendelezo utakuwa ni ule kuhusiana na kuboresha suala la uongozi Simba na kuingia katika suala la uwekezaji kama ambavyo mfanyabiashara Mohammed Dewji alivyojitokeza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV