November 12, 2016Unaweza kusema hii ni hali ya kushangaza, wachezaji watatu wa Taifa Stars, wameachwa nchini kutokana na kutokuwa na hati za kusafiria ‘passport’ kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Zimbabwe.

Kikosi cha Stars kimeondoka jana mchana kuelekea Zambabwe kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kesho Jumapili kwenye Mji wa Harare nchini humo.

Wachezaji walioachwa ni James Josephat kutoka Prisons, Said Kipao (JKT Ruvu) na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, huku Omar Mponda wa Ndanda akibadilishiwa ndege kutokana na passport yake kuchelewa, hivyo alitarajiwa kuondoka jana jioni.

Pale kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, lilishuhudia kikosi hicho kikiondoka huku changamoto nyingine ikiwa ni baadhi ya wachezaji nyota kusahau passport majumbani mwao.

Kuhusiana na hilo Mkwasa alisema kuwa licha ya kutofanya maandalizi ya kutosha, lakini anaamini watarudi na matokeo ya ushindi huku akithibitisha kuachwa kwa wachezaji hao.

“Tunakwenda kupambana kwa sababu malengo yetu ni kurudi na ushindi ambao utasaidia kutupandia katika viwango vya Fifa ingawa maandalizi yetu yamekuwa ni madogo sana,” alisema Mkwasa.


Kwa upande wake nahodha wa Taifa Stars anayekipiga Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta alisema: “Maandalizi kifupi yapo vizuri kwa sababu kila mchezaji ametoka kwenye ligi tuna imani tutashinda."

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV