November 23, 2016Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla, wakati wowote kuanzia sasa anaweza kuachana na timu hiyo na kwenda Ulaya kutafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa.

Meneja wa kiungo hiyo, Jamal Kisongo, amesema hivi sasa yupo katika harakati za mazungumzo na baadhi ya timu kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya ambayo yameonyesha nia ya kutaka kumchukua mchezaji huo.

Alisema endapo mipango hiyo itakaa sawa, muda wowote ataondoka nchini na kwenda huko kujaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa kama ilivyo kwa mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

“Said Ndemla muda wowote kuanzia sasa anaweza kuondoka zake nchini na kwenda Ulaya kwa ajili ya kujaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa kama alivyo Samatta.

“Hivi sasa nipo katika mazungumzo na baadhi ya timu ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka na endapo mambo yatakaa sawa basi ataondoka nchini kwa sababu tayari ameshakomaa kiakili na kifikra, hivyo anaweza kupambana,” alisema Kisongo.

Alipoulizwa kama uongozi wa Simba unaujua mpango huo, alisema: “Simba wanaujua, hivyo mambo yakikaa sawa ataondoka, wala hawana shida."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV