November 23, 2016



Kiungo na nahodha wa Yanga, raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima na beki wa pembeni wa timu hiyo, Hassan Kessy, wamemuwahi kocha wao mpya, Mzambia, George Lwandamina kwa kutimiza maagizo yake aliyowapa ya kufanya mazoezi binafsi kabla ya kuanza programu zake.

Agizo hilo alilitoa hivi karibuni mara baada ya kupata taarifa ya wachezaji wa timu hiyo kupewa mapumziko ya wiki mbili baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Mzambia huyo alitoa maagizo hayo kwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh kwa kuwataka awataarifu wachezaji wote kufanya mazoezi binafsi wakiwa mapumzikoni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema atatumia muda huu wa likizo kufanya kile anachotaka kocha wao kwa ajili ya kutengeneza fiziki na pumzi ili ligi itakapoanza awe fiti zaidi.

Niyonzima alisema ni ngumu kujipa nafasi ya kuwepo katika kikosi kutokana na ujio wa kocha mpya ambaye yeye anakuja na sera zake za aina ya uchezaji.
"Acha nikwambie kitu, ujue kila kocha anapokuja kwenye timu ni lazima aje na sera zake mpya, hivyo sijajua sera za huyo kocha wetu mpya.

"Ndiyo maana nimeona ni vyema nikawahi kujiweka fiti ili mara tutakapoanza mazoezi ya pamoja, niwe fiti zaidi ya hapa nilipo kwa kufanya mazoezi ya gym na uwanjani," alisema Niyonzima.

Kwa upande wa Kessy, yeye alisema: “Mimi siku zote napenda ushindani kwenye timu, hivyo ninayatumia vema mapumziko haya tuliyopewa kwa kujiweka fiti kwa kufanya mazoezi binafsi ya kukimbia milimani huku Morogoro nilipo.
"Pia kufanya mazoezi ya gym na uwanjani kwenye akademi yangu iliyonilea ya Moro Youth."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic