November 28, 2016

Timu ya Startimes Tanzania ikiongozwa na Waziri Sun kutoka China pamoja na uongozi wa runinga ya CCTV kutoka China, wamekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nauye.


Kwa pamoja na ujumbe huo mzito, walikutana na Nnauye kwenye hoteli ya Golden Tulip kabla ya kuhudhuria hafla ya pamoja iliyohusisha vyombo vya habari vya China na vile vya Afrika hasa Mashariki.

Katika hafla hiyo, Nnauye, Sun, viongozi wa CCTV na Startimes ambayo inafanya vizuri kwa sasa walipata nafasi ya kutoa nasaha zao na kuhimiza ushirikiano wa vyombo vya habari katika jamii hizo mbili yaani Afrika na China katika kuchagiza maendeleo ya kila upande.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV