November 29, 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na yule wa Chini ambaye ni Naibu Waziri wa Chama cha Ukomunisti, Sun Zhijun wamevitaka vyombo vya habari vya nchi zao kudumisha uhusianao wao kwa lengo la kuzisaidia jamii na kuhamasisha maendeleo.

Nnaye alikuwa mmoja wa waalikwa kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la vyombo vya habari vya China na vile vya Afrika Mashariki ambalo limeanza jana na litaendelea hadi Desemba 4 hadi katika mji wa Nairobi Kenya.

Nnauye alisema kama kutakuwa na ushirikiano wa sehemu mbalimbali ikiwemo katika suala la mafunzo, itakuwa chanzo cha maendeleo.

Zhijun naye alisisitiza hilo huku akisema ni nafasi nzuri ya kuboresha ushirikiano huo ambao umekuwepo miaka nenda rudi.


Kampuni ya Startimes ambayo ni maarufu kwa kuuza ving’amuzi bora hapa nyumbani na ukanda wote wa Afrika Mashariki, ndiyo wenyeji wa kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na waandishi mbalimbali kutoka China na nchi za Afrika Mashariki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV