December 20, 2016


Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amewataka wachezaji waachane na mgomo na warejee kazini.

Pamoja na kuwaomba wachezaji warejee kazini, ameutaka uongozi kukaa na kuzungumza na wachezaji wake.

Akilmali alikuwa akizungumzia suala la wachezaji kugoma na kusababisha kutofanya mazoezi kwa siku mbili, jana na leo kwa madai ya kutolipwa mshahara wa mwezi uliopita.

“Wachezaji lazima wajue mambo hayo hutokea, hivyo wanapaswa kurejea kazini na kuachana na mambo ya migomo. Wafanye kazi huku wakijua suala lao linaweza kushughulikiwa.

“Lakini uongozi nao ulishughulikie suala hili kwa kukutana na wachezaji wake na kulijadili suala hilo ili walimalize. Sisi kama viongozi tuko tayari kuwaunga mkono,” alisema Akilimali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic