TASNIA ya habari imepata pigo baada ya mpigapicha mwandamizi Mpoki Bukuku (44), kufariki dunia jana asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa zinasema Mpoki alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku baada ya kupata ajali ya gari eneo la Mwenge wakati akitokea kazini kwake The Guardian Limited, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Nilifanya kazi na Mpoki Mwananchi Communication Limited, mimi nikiwa upande wa Mwanaspoti naye akiwa mpigapicha mkuu wa kampuni hiyo.
Nilipata nafasi ya kushirikiana naye sana kwa kuwa mimi pia kitaaluma ni mpigapicha, hivyo mara kadhaa nililazimika kuwa ndani ya kitengo chake kuhusiana na masuala ya kamera na kadhalika.
Mpoki alikuwa rafiki, kaka wa aina yake. Alikuwa na maisha yake na nilimpenda zaidi kwa kuwa alitaka kuishi alivyotaka yeye na si kwa wanavyotaka wengine.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited, Richard Mgamba, kifo cha Mpoki kimetokea wakati bado mchango wake ukiwa unahitaji kwenye taaluma ya habari.
“Mpoki alikuwa ni mtu aliyeipenda fani yake na hakuogopa kupambana ili mradi apate habari nzuri. Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana kuna wakati kiu yake ya kupata habari nzuri kuliko wengine wote ilimuweka matatani,” alisema Mgamba na kuongeza;
“Mpoki alikuwa na sifa mbili za kupiga picha na kutafuta habari nzuri, alikuwa shujaa na mwenye mapenzi na kazi yake hasa wakati akifuatilia habari kubwa kokote kule katika nchi hii.”
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa jijini Dar es Salaam na ndugu, jamaa na marafiki.

0 COMMENTS:
Post a Comment