December 19, 2016


Kiungo James Kotei atakuwa vizuri ndani ya siku mbili hizi na tayari atakuwa amerejea mazoezini.

Kotei aliumia wakati Simba ikiivaa Ndanda FC na kutolewa nje kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Lakini Kote amesema anaendelea vizuri lakini bado atakuwa akifuata maelekezo ya daktari.

“Nasikia nafuu, lakini maumivu yalikuwa makali kwa kuwa alinigonga na kiwiko,” alisema.

Aliyemgonga ni mchezaji wa zamani wa Yanga na baadaye Simba, Kiggi Makasi ambaye alikuwa akiwania mpira na kiungo huyo Mghana.


Nafasi ya Kotei ilichukuliwa na Muzamiru Yassin ambaye baadaye aliifungia Simba bao la kwanza kabla ya Mohamed Ibrahim kufunga la pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic