December 19, 2016



Kocha George Lwandamina alipigwa na bumbuazi leo asubuhi baada ya wachezaji wake kugoma kuingia na kufanya mazoezi.

Wachezaji wa Yanga hawakufanya mazoezi kwa kuwa inaelezwa wanadai mishahara yao ya mwezi Novemba.

Mara baada ya wachezaji kutua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, walishindwa kuanza mazoezi.

Baada ya uchunguzi, iligundulika kwamba wachezaji hao walitaka kulipwa mishahara yao ya Novemba.
“Wachezaji hawajalipwa mishahara yao ya Novemba, hawataki kufanya mazoezi na kocha ameshindwa la kufanya,” alisema mmoja wa viongozi waliokuwa eneo hilo akithibitisha hilo na kusisitiza yeye si msemaji.

Juhudi za kumpata Katibu Mkuu, Barala Deusdedit ziligonga mwamba, kama ada simu yake huita bila ya kupokelewa hata pale anapotumiwa ujumbe kuelezwa kusaidia kutoa ufafanuzi wa jambo, huwa hajibu.

Wachezaji Yanga wamefanya hivyo ikiwa ni siku moja tokea waanze Ligi Kuu Bara hatua ya mzunguko wa pili kwa kishindo wakiitwanga JKT Ruvu kwa mabao 3-0.


2 COMMENTS:

  1. sasa kama alkwambia yy si msemaji wa timu, alikupatia taarifa hiyo akiwa kama nan?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic