December 28, 2016



Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameibuka na kusema kiungo wao, Mzambia, Justine Zulu, bado hajawa fiti kucheza kwa kiwango chake na ndiyo maana mpaka sasa hajapewa nafasi kubwa ya kuitumikia timu hiyo.


Zulu aliyekuwa akiitumikia Zesco ya nyumbani kwao kabla ya kutua Yanga, bado hajafanikiwa kucheza mechi yoyote ya ligi kati ya mbili ambazo tayari Yanga imeshacheza tangu aje yeye, lakini alicheza mechi moja ya kirafiki tena akitokea benchi.

Mzambia huyo aliyekuja kuchukua nafasi ya Mnyarwanda, Mbuyu Twite aliyemaliza mkataba wake na Yanga, alikosa mechi ya kwanza dhidi ya JKT Ruvu kutokana na kukosa kibali cha kazi, lakini mchezo wa pili dhidi ya African Lyon, aliishia kukaa benchi licha ya kukipata kibali hicho.


“Zulu bado hajawa fiti kwa sababu hakuweza kucheza soka kwa takribani miezi sita kutokana na kufungiwa na shirikisho la soka la kwao, hivyo anahitaji muda zaidi wa kurudisha kiwango chake kabla ya kuanza kuitumikia rasmi timu yake mpya.

“Lakini kadiri siku zinavyokwenda, uwezo wake unaanza kurudi na siku si nyingi ataanza kuonekana uwanjani, mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kuhusiana na yeye,” alisema Mwambusi.


Ikumbukwe kuwa, Zulu alifungiwa kutocheza soka kwa miezi sita na shirikisho la soka la nyumbani kwao baada ya kuingia kwenye mgogoro na wakala wake.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic