December 28, 2016




Klabu ya Zesco ya Zambia imeitangaza kupitia moja ya gazeti la nchini humo, nafasi ya Kocha Mkuu kuwa iko wazi.

Nafasi hiyo iko wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, George Lwandamina kupata kazi Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara.

Zesco imetangaza kwa yoyote aliye na uwezo wa kuwania nafasi huyo huku ikiweka vigezo.

Moja ya vigezo ilivyoweka ni kuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka mitano, kuwahi kufundisha moja ya klabu kubwa kwa mafanikio au kuwa mmoja wa makocha wa timu ya taifa.

Zesco ni moja ya klabu kubwa za Zambia zinazochipukia baada ya vigogo kama Mufulula Wanderers,  Dynamo na Zanaco.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic