December 28, 2016



Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameibuka na kusema kuwa, timu ya Yanga ambayo wamepangwa nayo kundi moja kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, ndiyo itakuwa kipimo chao kikubwa kama wapo fiti.

Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 30, mwaka huu visiwani Zanzibar, Azam na Yanga zimepangwa Kundi B sambamba na Zimamoto na Jamhuri.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema: “Kocha wetu Zeben tayari amekiandaa vizuri kikosi chake na amebaini kwamba kundi letu ni gumu kutokana na timu zilizopo ikiwemo Yanga.

“Kama tujuavyo, Yanga inapokutana na Azam kunakuwa na ushindani wa hali ya juu, hivyo amesema ni kipimo sahihi kwa wachezaji wake kuonyesha umahiri wao, ikiwezekana kuwa mabingwa kabisa.”

Aidha Idd alisema kikosi chao kinatarajiwa kwenda visiwani humo Ijumaa au Jumamosi baada ya kumaliza mechi yao ya ligi kuu dhidi ya Prisons itakayopigwa Alhamisi usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic