December 17, 2016

 

MCHEZO UMEMALIZIKA

Dakika 90 + 4: Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inatoka kifua mbele kwa kuwa na mabao 3-0. Licha ya mabao yaliyofungwa na Msuva lakini Niyonzima alikuwa na mchango mkubwa katika mabao yote na ameonyesha uwezo mkubwa katika dakika zote 90.

Dakika ya 90 + 4: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Ngoma anaingia Chirwa.

Kazi nzuri iliyofanywa na Haruma Niyonzima kutoka katikati ya uwanja, anaingia na mpira na kupiga pasi nzuri kwa Muva ambaye anamlizia kwa kupiga shuti la kumchambua kipa wa Ruvu.

Dakika ya 90 + 3: GOOOOOOOOOOO MSUVAAAAAAA

Dakika ya 90 + 2: Yanga wanapiga pasi safi nje ya lango la Ruvu na kupata shangwe kubwa hapa uwanjani lakini wanashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya kwa kuruhusu walinzi wa Ruvu kuokoa mpira.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.

Dakika ya 89: Ngoma anapata nafasi ya kupiga shuti langoni mwa Ruvu, anafanya hivyo lakini linakosa nguvu na kipa wa Ruvu analidaka.

Dakika ya 87: Muda mwingi kocha wa Yanga, Lwandamina amekaa kwenye benchi na hajanyanyuka kutoa maelekezo kama ambavyo makocha wengi wamekuwa wakifanya.

Dakika ya 85: Yanga wanafanya mabadiliko, ametoka Thaban Kamusoko ameingia, Mwashiuya.


Dakika ya 79: Haruna Niyonzima anawachambua walinzi wa Ruvu nje ya eneo la 18 la lango la wapinzani kisha anapiga shuti kali linamgonga mlinzi wa Ruvu na kutoka nje, inakuwa kona ambayo haikuwa na faida.


Dakika ya 75: Ruvu wanapata kona, inapigwa lakini Dida anatumia urefu wake kuudaka.



Dakika ya 73: Rahim Juma wa Ruvu anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.



Dakika ya 70: Bossou anagongana na beki wa Ruvu, analala na mwamuzi anaamua apatiwe matibabu, mchezo umesimama kwa muda.


Dakika ya 67: Mchezo umeanza kutawaliwa kwa mashambulizi kadhaa ya kupokezana, Yanga wanajaribu kujipanga kwa kupitia pembeni.


Dakika ya 65: Ruvu wanafanya mabadiliko, anatoka Ally Billal anaingia Mussa Juma.

Dakika ya 63: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini washambuliaji wao wanakosa umakini katika umaliziaji.

Dakika ya 59: Ruvu wanajaribu kujibu mapigo kwa kufanya shambulizi kali lakini Dida anafanya kazi nzuri kwa kuudaka mpira.
 
Dakika ya 57: Msuva anafunga bao zuri kwa kichwa, ni baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Haruna Niyonzima kutoka upande wa kulia wa uwanja.



GOOOOOOOOOO MSUVAAAAAAA


Dakika ya 56: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Tambwe anaingia Said Juma Makapu.



Dakika ya 52: Yanga tena wanafanya shambulizi kali kwa kupiga shuti kali langoni lakini kipa analipangua na kutoka nje, inakuwa kona. Baada ya hapo kipa akalala chini na kuonyesha kaumia mkono.



Dakika ya 52: Amissi Tambwe anakosa nafasi ya wazi, anabaki yeye na kipa wa Ruvu lakini beki wa Ruvu anamuwahi na kuharibu mpira ambapo shuti linatoka nje.



Dakika ya 51 : Mchezo bado hauna kasi kubwa, Yanga wanafanya mashambulizi lakini yanakosa nguvu.



Dakika ya 48: Msuva anachezewa faulo na mlinzi wa Ruvu, amelala chini anapatiwa matibabu. Mchezo umesimama kwa muda.



Dakika ya 47: Ruvu wanajipanga na kufanya shambulizi kwa kupiga shuti kali lakini linadakwa na Dida.



Yanga bado inaongoza bao 1-0, mchezo umeanza kwa kasi ndogo kiadi, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Ruvu.



Kipindi cha pili kimeanza.


MAPUMZIKO


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA


Dk 44, Bado na JKT bado wanaendelea kushambulia lakini hawako makini

Dk 39 hadi 41, JKT wanaonekana kubadilika na kushambulia lakini hakuna mashambulizi makali sana


GOOOOOOOOO Dk 38, Michael Aidan wa JKT anaukwamisha mpira langoni mwake wakati akiokoa krosi ya Msuva

Dk 37, Ngoma anapoteza nafasi nzuri kabisa akiwa katika eneo zuri

KADI Dk 35 Edward Charles analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva

Dk 30, pasi nzuri ya Niyonzima, Msuva anapaisha akiwa sentimeta chache kutoka lango la Yanga

Dk 24 hadi 27, JKT nao wanaonekana kuamka na kucheza kwa kushambulia. Lakini Yanga wanaweza kuingia kwenye lango la JKT zaidi


Dk 22, Tambwe anainganisha krosi ya Niyonzima kwa kichwa, lakini kipa anadaka kwa ulaini

Dk 19, Atupele anamtoka Yondani na kuachia mkwaju mkali, unagonga mwamba wa juu na kutoka


Dk 15, JKt wanaanza kufunguka ingawa Yanga wanaonekana wako vizuri ingawa hawana kashkash kubwa langoni mwa JKT

Dk 14, JKT wanapata kona, Najib Magulu anaichonga vizuri lakini Yanga wanaokoa

KADI Dk 12 Yusuf Juma analambwa kadi ya njano kwa ajili ya kumuangusha Msuva


Dk 8, Niyonzima anaingia vizuri kabisa, lakini mabeki JKT wanalazimika kumuangusha

Dk 6, Yanga inapata kona yake ya kwanza, Juma Abdul anachonga lakini JKT wanaokoa hapa. Ilikuwa hatari.

Dk 4, Kelvin Nashon anajaribu kuingia lakini Yanga wanaonekana kuwa makini.

Dk 2 Tambwe anaingia vizuri lakini anawekwa chini hapa.


Dk 1, Yanga ndiyo wanaanza kushambulia kwa kasi lakini JKT wanakuwa makini.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic