Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ametamka kwamba wana kila sababu ya kushinda kwenye mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Ndanda FC kutokana na ubora walionao kuliko wapinzani wao.
Simba, kesho itaanza mechi za mzunguko wa pili ikiwa ugenini mkoani Mtwara kucheza na wenyeji Ndanda, mechi itakayopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mayanja amesema kwamba kikosi hicho kimekuwa na maandalizi mazuri pamoja na kurekebisha dosari kwenye kikosi hicho kwa kufanya usajili mzuri.
“Uhakika wa kushinda mbele ya Ndanda ni mkubwa sana kutokana na ubora uliopo baina yetu na wapinzani wetu Ndanda ambao kila tunapokutana nao wamekuwa dhaifu.
“Maandalizi tuliyoyafanya pamoja na usajili huu wa dirisha dogo ni miongoni mwa vitu ambavyo vinatupa nafasi ya kuona kwamba tutaendelea kufanya vizuri kama ilivyokuwa mzunguko wa kwanza,” alisema Mayanja.







0 COMMENTS:
Post a Comment