| KOTEI |
Kiungo mpya wa Simba, James Kotei amesema anaamini kutakuwa na ushindani mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara na ndiyo kitu anachokihitaji.
Kotei raia wa Ghana ambaye amejiunga na Simba siku chache zilizopita, amesema anachotaka ni ushindani wa kimpira ili umkuze.
"Naamini kutakuwa na ushindani wa juu kabisa. Nataka hilo jambo, hauwezi kukua bila ya kuwa na ushindani," alisema.
"Simba ina kikosi bora, wachezaji vijana ni wengi. Maana yake ushindani unaanzia kikosini halafu unakwenda kwenye timu pinzani. Hili ni jambo zuri kwa anayetaka kukua zaidi."
Simba tayari iko mjini Mtwara kwa ajili ya mechi yake ya kwanza ya mzunguko wa pili Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijao na Kotei kama ataanza itakuwa ni mechi yake ya kwanza.







0 COMMENTS:
Post a Comment