Na Saleh Ally
SUALA la
ushirikina katika soka limekuwa likizungumzwa kama hadithi za kufikirika, wako
ambao wanasema mambo hayo hayatokei, lakini wako ambao wamekuwa wakithibitisha
kuwa hali hiyo inatokea.
mu mbalimbali, mfano
wachezaji kwenda kwa waganga wa kienyeji maarufu kama wataalamu na kufanya kitu
fulani ili kuwadhoofisha wenzao au wachezaji wanaocheza nao katika kikosi
kimoja.
Wako ambao wamekuwa wakifanya kila
linalowezekana kuhakikisha wachezaji wenzao wanaumia, katika soka suala hilo ni
maarufu kama ‘misumari’ wakiwa na maana kuwa anayeumizwa, basi anakuwa amepigwa
misumari.
Uchunguzi wa Championi kwa takribani mwezi
mmoja na ushee, limekuwa likizunguka sehemu mbalimbali kufanya uchunguzi, ishu
kubwa ilikuwa ni kuzungumza na watu mbalimbali na kutaka kujua kuhusiana na
suala la ushirikina.
Inaonekana pamoja na kuwa na mambo mengi,
suala hilo limegawanyika kwenye mambo mengi lakini matatu ndiyo yanaonekana
kuchukua nafasi. Kwanza ni kuroga ili kuhakikisha timu inashinda, lengo hapa ni
kuidhoofisha timu moja ili nyingine ishinde.
Suala la pili ni mchezaji kuhakikisha mmoja
anaumia na kushindwa kabisa kufanya vizuri ili kumpa nafasi yeye aendelee
kufanya vizuri na la tatu, mchezaji ni kusafisha nyota yake na kuidhoofisha ya
mwenzake na hapo yeye atang’ara na kufanikiwa huku yule mwingine akifeli.
Katika watu mbalimbali ambao walifanya
mahojiano na Championi Ijumaa, wengi wakiwa kutoka katika klabu kubwa za Simba,
Yanga, Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union, wamekiri kuwa kweli ushirikina
hufanyika.
“Hauwezi kusema uache kufanya ushirikina,
sisi tumekuwa tukifanya kwa lengo la kujilinda na kupambana na timu pinzani.
Kama wenzetu wanafanya hivyo, sisi tukikaa kimya maana yake tunakubali kuumia,”
anasema mdau mmoja kutoka moja ya klabu kubwa za Tanzania.
“Uongozi unatutambua, kumekuwa hadi na
fungu letu na lengo ni zuri tu, kuilinda timu yetu na kuisaidia kufanya
vziuri, kamwe hatulengi kumuumiza mtu,” anasisitiza.
Rekodi ziko nyingi sana kuhusiana na
masuala ya ushirikina, hadi wachezaji Waafrika wale maarufu wanaocheza Ulaya
kama Didier Drogba, Samuel Eto’o na wengine wamekuwa wakihusishwa na kufanya
hivyo.
Mwaka 2009, mwandishi wa makala haya,
alishuhudia baadhi ya waganga wa kienyeji nchini Ivory Coast wakiishi maisha ya
juu kutokana na mamilioni ya fedha wanayoingiza.
Uchunguzi wake ulionyesha kuwa wana fedha
nyingi kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi ya kusafisha nyota za wachezaji maarufu
wa nchini hiyo wanaocheza Ulaya kama Yaya & Kolo Toure, Drogba, Didier
Zokora, Aruna Dindane na wengine.
Hapa vipi kuhusiana na suala hilo,
Championi likaanza kukata mbuga likisaka mganga wa kienyeji ambaye amewahi
kuifanya kazi yake hiyo vizuri kwa lengo la kuwasaidia wachezaji kuosha nyota
zao.
Uchunguzi ulionyesha mganga huyo kijana na
maarufu anapatikana eneo moja la vitongoji vya Jiji la Dar es Salaam na kazi ya
kutafuta namba yake ikafanyika kupitia ndugu yake. Baada ya makubaliano, siku
ya kwenda ‘kumtibu’ mchezaji huyo ikapangwa.
Waandishi wawili wa makala haya, Saleh Ally
akajitambulisha kama meneja anayeishi barani Ulaya na mchezaji, Sweetbert
Lukonge ndiye mchezaji anayetaka kwenda kucheza Ulaya, alitaka nyota yake
ing’are kuanzia hapa nchini, baadaye Ulaya.
Miadi ikatengwa na siku ilipowadia, Meneja
(Saleh) ambaye lafudhi yake kidogo ina Kiswahili cha shida kutokana na kuishi
Ulaya siku nyingi pamoja na mchezaji (Lukonge) walifika kwenye kitongoji hicho
na kupokelewa. Moja kwa moja, wakafikishwa hadi nyumbani.
Gari walilazimika kulipaki barabarani,
halafu wakaingia mitaa ya ndani (si mbali sana) ambako gari halifiki na kwenda
nyumbani kwa mganga huyo kijana, mahiri ‘kuwaponya’ wachezaji ili waweze
kufanya vizuri katika soka.
Baada ya kufika, mganga aliuliza shida yao,
maelezo ya meneja yalilenga kumsaidia mchezaji huyo ili amfunike mchezaji
mwingine ambaye alikuwa akimzuia kupata namba kwa kuwa huyo meneja anataka
mchezaji wake ang’are.
Mganga aliwahakikishia kuwa kila kitu safi
kabisa na ndani ya siku chache baada ya tiba ya siku hiyo. Mambo yangekuwa
mazuri lakini kulikuwa na bidhaa za kununua siku hiyo ili kuanza tiba.
Vifaa vilivyotakiwa ni kuku wawili, weupe
na weusi, kitambaa, kipande cha sanda ambacho kimefukuliwa baada ya mtu
kuzikwa. Yai na vingine ambavyo tayari viliandaliwa na mganga huyo.
Ikatolewa Sh 20,000 kwa ajili ya kununuliwa
kuku wawili na bei ya ‘matibabu’ hayo ilikuwa ni Sh 300,000 hadi 400,000 ingawa
kulikuwa na makubaliano kwa vile mganga anaonyesha si mtu wa tamaa na anayetaka
‘kusaidia’ watu.
Makubaliano yanafikiwa, meneja na mchezaji
wake wanalazimika kumsubiri mganga anayefunga safari kwenda kununua kuku, baada
ya kurejea anaomba muda mchache kuandaa vifaa vyake kabla ya kuanza kazi.
Baada ya hapo, mtoto mdogo anatumwa kuwaita
wahusika (meneja, mchezaji) ambao baada ya kuingia kwenye chumba ambacho
hufanyika kazi za mganga wanaelezwa kazi itakavyofanyika chumbani humo na baada
ya hapo ni safari ya kwenda makaburini ili kuimaliza kazi hiyo huko.
Kidogo wawili wanaingiwa hofu, lakini
mganga anawasisitiza hawapaswi kuwa waoga hata kidogo kwa kuwa kila kitu
kitakwenda vizuri huku akiwatolea mfano wachezaji maarufu wa Yanga, Simba na
timu nyingine ambao wamewahi kufika na kupata tiba hiyo ya kuosha nyota.
“Hata watu wa kawaida na maofisa wanafika
hapa kwa ajili ya kupata huduma hii, ondoeni hofu na mambo yatakwenda vziuri,”
anasema mganga huyo kijana.
Suala la makubaliano ya bei linafanyika na
anakubali kupunguza bei ingawa wahusika ni watu wanaoishi ‘Ulaya’.
Na kwa nafasi hiyo, meneja anaomba
kupiga picha za kumbukumbu ambazo ataenda nazo Ulaya kwa kuwa kule ni mambo
tofauti na huenda itamsaidia ‘fundi’ kupata wateja zaidi kutoka ughaibuni.
Anapewa ruhusa.
Kazi inaanza, mchezaji anakalishwa kwenye
kigoda (lazima akae kwenye kiti juu, ili nyota yake ipande), anafunikwa shuka
lenye rangi nyeupe). Kazi inaanza.
Mganga huyo au fundi anachukua vitu kama
ukindu anavifunga na kufunga kwenye miguu ya mchezaji ambaye amevaa jezi ya
Liverpool, butka nyeupe na viatu Adidas rangi ya njano. Anachukuliwa kuku
mweupe na mweusi anaachwa pale chini.
Yule kuku mweupe, huku ubani umefukizwa
kwenye chetezo kikubwa kama bakuli, moshi unaanza kufuka. Mchezaji anamchukua
kuku huyo na kumuweke kwenye moshi unaofuka, ghafla kuku analala kama mlevi
aliyezidiwa kinywaji na anafanya hivyo huku akitakiwa kunuwia anataka apate
nini, anafanya hivyo.
Wakati huo, mganga anaendelea kuandika
majina ya viongozi wa timu ya mchezaji huyo ambao wanatakiwa kumsahau yule
mchezaji mwingine na kumfikiria mchezaji aliyeletwa na meneja.
Baada ya hapo, karatasi lenye majina anakabidhiwa
mchezaji huyo mkononi. Halafu analiweka juu ya moshi unaofuka kupitia chetezo,
na mganga anachukua dawa aina mbili pamoja na mafuta fulani hiyo, anamwaga juu
ya karatasi na ghafla moto unalipuka.
Meneja jasho linamtoka na mchezaji
halikadhalika anaonyesha kuwa na hofu kuu. Lakini mganga anaendelea na kazi
yake kwa ustadi mkubwa huku akisisitiza wakati huo ndiyo mwanzo kabisa kazi
inaanza kwani kuna mengi kama kumlisha kitu kuku na kumchinja, pia kwenda
makaburini kuchimbia vitu kwenye makaburi.
MAKALA HII ILIANDIKWA KWA MARA YA KWANZA
KWENYE GAZETI LA CHAMPIONI NA BAADAYE KUTOKA KWENYE BLOG YA SALEHJEMBE.











Mwisho wake ikawaje
ReplyDeleteMwisho wake ikawaje
ReplyDelete