| BAADA YA MECHI... |
Crescentius Magori ni kati ya wanachama wakongwe wa kundi la Friends of Simba (FOB).
Juzi alionekana ni mwenye furaha kuu mara tu baada ya mechi kati ya Simba dhidi ya Ndanda FC kumalizika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Simba ilikuwa imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 na Magori ambaye aliwa kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alionekana ni mwenye furakha kweli.
Hata hivyo, furaha ya Magori ilifuatiwa na subira, kwani awali hakuwa hivyo na wenyeji Ndanda FC walionekana walipania kushinda mechi hiyo.
Lakini mwisho, Simba wakaonyesha kiwango na kufanikiwa kushinda.
Kabla, Magori akiwa na wanachama wengine na viongozi wa Simba kama Muslah Al Rawah na Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' walionekana kuwa watulivu wakifuatilia mchezo kwa umakini kabisa.
| WAKATI MECHI IKIENDELEA |







0 COMMENTS:
Post a Comment