Ndanda si timu nyepesi, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wanalijua hilo, ndiyo maana hawataki mchezo.
Chini ya Kocha George Lwandamina, Yanga wameendelea na mazoezi yao kujiwinda kuivaa Ndanda FC kesho.
Kocha Lwandamina anajua mechi haitakuwa laini. Kikosi chake kimeendelea na mazoezi kwa umakini mkubwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga wanajua wana deni, hasa baada ya kuambulia sare katika mechi iliyopita dhidi ya African Lyon, watataka kushinda mechi ijayo.







0 COMMENTS:
Post a Comment