January 23, 2017Hata kama bado atakuwa hajawafurahisha sana mashabiki wa Arsenal lakini kiungo Mesut Ozil ndiye mchezaji bora zaidi ndani ya Ujerumani katika kipindi cha miaka 10.

Ozil anakuwa bora zaidi nchini humo kwa kuwa amefanikiwa kubeba tuzo ya mwanasoka Bora wa Ujerumani kwa kutwaa tuzo hiyo mara tano katika miaka sita.


Kama unavyoijua Ujerumani ni nchi yenye wachezaji bora kabisa. Lakini Ozil, ameendelea kuwa bora zaidi akiwazidi wengi ambao wanajulikana pia ni bora zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV